JULIO: YANGA WATAIFUNGA SIMBA
Kocha wa Dodoma FC ambaye ameshawahi kuichezea na kuifundisha Simba, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, amefunguka kuwa Yanga wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo Jumamosi kutokana na watu wengi kuwadharau.
Yanga atakuwa dimbani kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ambao unategemewa kuwa na ushindani huku wadau wengi wakiipa nafasi zaidi Simba kuibuka na ushindi hasa kutokana na matokeo ya bao 1-0 waliyovuna kwa Al Ahly.
Kwa mujibu wa Championi, Julio alisema kuwa watu wasiidharau Yanga kwa sababu ya ushindi wa Simba dhidi ya Waarabu, kwa kuwa historia ya michezo hiyo inaonyesha kwamba timu inayoonekana dhaifu ndiyo inapata ushindi.
“Simba atafungwa hii mechi kwa sababu wachezaji na benchi la ufundi wamezidi kujiamini sana kutokana na kuwa na kikosi kipana, lakini kubwa ushindi waliopata dhidi ya Waarabu.
“Wanasahau kuwa michezo ya Simba na Yanga huwa haitabiriki na mara nyingi timu ambayo inaonekana mbovu ndiyo upata matokeo ya ushindi,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment