February 16, 2019


SIMBA huenda ikapata pigo la kumkosa beki wake ‘mtukutu’, Mganda Juuko Murshid aliyeandaliwa maalum kwa ajili ya kumdhibiti staa wa Yanga, Heritier Makambo baada ya beki huyo kupata majeraha ya mfupa wa mbele wa mguu (ugoko).

Juuko aliandaliwa kwa ajili ya kumdhibiti Makambo leo Ju­mamosi wakati timu za Simba na Yanga zitakapokutana katika Ligi Kuu Bara.

Mganda huyo ambaye anasifika kwa soka la kucheza kibabe mbele ya washambuliaji mahiri alipata majeraha hayo ya ugoko wakati wa mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Al Ahly ikiwa ni ya Ligi ya Mab­ingwa Afrika.

Mganda huyo jana hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba am­bacho kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa Yanga.

Juuko hakufanya mazoezi hayo akiwa sambamba na Nyoni na Asante Kwasi ambao nao ni majeruhi.

Licha ya Championi Ijumaa, kumuuliza Daktari wa Simba, Yassin Gembe juu ya majeraha ya Juuko lakini alikataa kuzun­gumzia. “Hizi mechi za Simba na Yanga sisi hatuzungumzii kitu chochote, waulizeni vion­gozi,” alisema Gembe.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic