February 11, 2019


KOCHA mwenye mbinu ngumu kwa makocha wenye asili ya uzungu, Seleman Matola amesema kuwa kikosi chake hakina hela ila atapambana kuwamaliza matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC.

Matola amewapa taabu makocha wote wenye asili ya uzungu ikiwa ni pamoja na Hans Pluijm alipokutana naye mzunguko wa kwanza kwa kulazimisha suluhu Uwanja wa Chamazi na mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems kwa kutoa naye suluhu Uwanja wa Taifa.

Matola amesema anashukuru wachezaji wake wanamuelewa na wanafanya kazi kwa juhudi wakiwa uwanjani hali inayomfanya azidi kujisikia faraja kuwa nao.

"Hatukutegemea kuwa katika hali kama hii kwenye Ligi Kuu Bara hasa baada ya kuwakosa wadhamini, timu inapitia katika mazingira magumu ila wachezaji wamekubaliana na hali wanapata matokeo uwanjani.

"Benchi la ufundi tulikaa na wachezaji tukawajenga kisaikolojia na akili zao zikaelewa sasa ni mwendo mdundo, tutakutana na wapinzani wetu ambao wapo vizuri kiuchumi ila nina imani tutabakiza pointi zetu hapa," amesema Matola.

Lipuli inashika nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 24 ikiwa imekusanya pointi 36 leo itakuwa Uwanja wa Samora kumenyana na Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic