February 16, 2019


WAKATI leo Jumamosi, Yanga ikitarajiwa kupambana na Simba, tayari kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameshapata kikosi cha kwanza kitakachoanza katika mchezo huo.

Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 58, itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga ambacho kilipiga kambi mkoani Morogoro tangu Jumatatu ya wiki hii, kili­kuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia uliopo Bigwa japo hivi sasa kipo Dar tangu juzi usiku.

Katika mazoezi ya Morogoro majira ya asub­uhi, Zahera raia wa DR Congo, alionekana kuwa makini na kikosi ambacho kinaaminika ndicho kitaanza katika mchezo huo wa leo.

Kikosi hicho kilikuwa kinaun­dwa na Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Heritier Makambo, Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu.

Zahera aliwagawa wache­zaji wake kwenye vikosi viwili ambapo kikosi hicho wachezaji wake ndiyo walionekana kuwa ndiyo wana nafasi kubwa ya kuanza.

Wakati huohuo, Zahera aliamua kuchukua maamuzi magumu baada ya kuagiza kiko­si chake kirejee Dar jana jioni.

“Kocha kasema sababu kubwa ni kuwa hataki wachezaji wa­choke, amehisi wakisafiri Ijumaa (juzi) kurudi Dar wanaweza kuwa na uchovu wakati wana mch­ezo muhimu, hivyo muda huu (jana jioni) ndiyo tunarudi Dar,” alisema mtoa taarifa aliyekuwa na timu kambini Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic