MCHEZO wa leo wa Yanga na Simba utakaopigwa Uwanja wa Taifa ambao umebeba hisia kubwa za mashabiki utaibua majembe mapya matatu ambayo mzunguko wa kwanza hayakuwa na vikosi vya timu hizo.
Katika mchezo wa leo Yanga wanaonekana kuwa na vifaa viwili vipya ambavyo kama kocha Mwinyi Zahera ataamua kuvitumia basi itakuwa ni mara yao ya kwanza kucheza mchezo wa Kariakoo Derby.
Haruna Moshi 'Boban' huyu alikuwa African Lyon lakini kwenye dirisha dogo alijiunga na Yanga ameshaanza kuonyesha makeke yake ndani ya ligi pia Issa Mohamed 'Banka' alikuwa nje kutokana na adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa muda wa miezi 14 tayari amemaliza adhabu yake.
Kwa upande wa Simba wao hawakuwa na mbwembwe nyingi dirisha dogo walimsajili jamaa anaitwa Zana Coulibaly wanamwita mzee wa kumwaga maji tayari ameshaanza kuonyesha makeke yake ila leo itakuwa ni mara ya kwanza kucheza Kariakoo Derby.
0 COMMENTS:
Post a Comment