STRAIKA SIMBA AMJAZA NOTI ZA MAANA SHABIKI
PASI aliyoitoa mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwa Meddie Kagere wakati walipocheza na Waarabu Al Ahly, juzi Alhamisi ilimnufaisha shabiki wa Simba baada ya kushinda kiasi cha Sh 26,000 ikiwa ni kutokana na kuibuka kwa mvutano baina yake na shabiki mwenzake.
Shabiki huyo, Peter Mussa alijipatia kiasi hicho kwenye mazoezi ya Simba, jana kwenye Uwanja wa Boko ikiwa ni baada ya kumshinda mwenzake ambaye waliweka dau la kiasi cha Sh 13,000 baada ya kuzuka kwa ubishani juu ya pasi ya Bocco kwenda kwa Kagere alitoa kwa kichwa au kifua.
Mashabiki hao walianza kubishana kwa muda mrefu juu ya pasi aliyoitoa Bocco kwenye mechi ya Al Ahly wakati wa mazoezi ya timu hiyo yakiendelea kabla ya mwisho ubishani wao kumalizwa na Bocco mwenyewe.
Baada ya mazoezi kumalizika Bocco aliulizwa na mashabiki hao wakitaka kujua ni namna gani alivyotoa pasi hiyo kabla ya kujibu aliitoa kwa kichwa na kumfanya shabiki huyo ajipatie kiasi hicho cha Sh 26,000 lakini akaamua kutoa Sh 5,000 akampa Bocco kama zawadi kwa kumaliza ubishi.
0 COMMENTS:
Post a Comment