February 17, 2019



KIKOSI cha Simba leo kimetia timu jijini Arusha baada ya kuondoka asubuhi kwa ndege kupitia Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Simba wamepokelewa kishujaa na mashabiki wa Arusha baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere dhidi ya watani wao Yanga mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa.

Simba hawakutaka kupumzika leo kwani walianza mazoezi jioni kwa ajili ya kurejesha miili sawa.

Simba watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon utakaochezwa Jumanne ya Februari 19, Uwanja Amri Abeid.

1 COMMENTS:

  1. Mayebo waache kulalama kila kukicha, ndege za Magufuli silo bwerereee, kwa nini hawataki kutumia huu usafiri rahisi na wa haraka?

    Wanaombea tiefuefyu wasimamishe ligi na kuamuru timu inatoongoza ligi itangazwe bingwa. Thibuutuuuuu, ndoto y’a mchana!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic