February 11, 2019

MKONGWE ndani ya timu ya Manchester United, Peter Schmeichel anaamini kwamba Jose Mourinho alikosa sapoti kutokana na ushawishi wake kuwa mbaya.
Schmeichel amesema Manchester walijadili na kutafuta sababu kwa nini Mourinho anashindwa kupata matokeo mazuri. 
"Nadhani ni tatizo kubwa sana ambalo lilikuwa linamsumbua ni suala zima la mawasiliano.
"Alikuwa anaiwakilisha Manchester United lakini hakuwa akifanya vizuri hasa katika mawasiliano jambo ambalo limepelekea kuondolewa kwakwe.
"Kuna mashabiki zaidi ya milioni wa Manchester United kila mahali ulimwenguni wapo, walikuwa wanahitaji Meneja ambaye anauwezo wa kushawishi," amesema Schemeichel.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic