February 15, 2019




BAO la Meddie Kagere Uwanja wa Taifa dakika ya 64 dhidi ya Al Ahly ya Misri lilifufua matumaini ya Simba kusonga mbele kimataifa.

Simba walishinda mchezo wao wa pili kwenye hatua ya makundi baada ya kuboronga kwenye michezo miwili kwa kuchapwa mabao 10 walipokuwa ugenini.

Rekodi zinaonyesha kuwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly Uwanja wa Taifa ulikuwa ni wa kistaarabu kwa Simba kwani hawajazoea kumchinja mpinzani wao Taifa kwa bao 1-0.

Simba walitinga hatua ya awali baada ya kumchinja Mbabane Swallows Taifa kwa mabao 4-1, pia walimchinja Nkana FC Uwanja wa Taifa mabao 3-1, walipoccheza na JS Saoura waliichinja mabao 3-0 Taifa na kipigo cha Al Ahly cha bao 1-0 ni cha kistaarabu kwao.

Matokeo hayo yanaifanya Simba ifikishe jumla ya pointi sita huku Al Ahly yenye pointi saba nafasi ya kwanza mchezo wao unaofuata ni dhidi ya JS Saoura ugenini Marchi 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic