February 15, 2019


KOCHA mkuu wa Tanzania Prisons, Adolf Richard amesema bado wachezaji wake wana tatizo katika umaliziaji hali ambayo inamfanya akae nao chini kuzungumza nao upya.

Prisons kwa sasa imekuwa na matokeo chanya tofauti na mzunguko wa kwanza kwani imefanikiwa kupata ushindi mara mbili mfululizo baada ya kushinda mbele ya Mbao FC jana iliinyoosha Azam FC kwenye Uwanja wa Sokoine.

"Tunacheza kwa kujiamini na kutengeneza nafasi, tatizo kubwa linakuwa kwenye kumalizia ndio maana mchezo wetu dhidi ya Azam tumepata bao la penalti, ila ni kitu kizuri kwa timu kupata matokeo nina imani itabadilika hivi karibuni," amesema Richard.

Prisons inashika nafasi ya 14 baada ya kucheza michezo 26  na kujikusanyia pointi 29 imepanda kwa nafasi mbili kwani awali ilikuwa nafasi ya 17, pia ni miongoni mwa timu iliyodumu muda mrefu nafasi ya 20 kwa mzunguko wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic