Shabiki wa klabu ya Yanga, Frank Kayombo mkazi wa Njombe ameibuka mshindi wa milioni 188.5 baada ya kubashiri vyema timu 12 (Perfect 12) ya Kampuni ya Kubashiri ya M-Bet.
Kayombo amekuwa mshindi wa kwanza wa Perfect 12 kwa mwaka 2019 akijinyakulia kiasi hicho cha fedha baada ya mwaka uliopita kupatikana washindi 22.
Akizungumzia ushindi wake Kayombo amesema kwenye fedha hizo ataichangia klabu yake ambayo iko katika matatizo ya kiuchumi.
"Nimefurahi kushinda Perfect 12, mara ya kwanza nilikuwa ninashinda fedha za kawaida tofauti na hii, sikuwa ninaamini lakini kwa sasa ninawaambia wengine waendelee kucheza kupitia M-Bet.
"Nimekuwa nikicheza tangu 2014, ushindi huu nimeupata baada ya kucheza Februari 8, mwaka huu, kikubwa baada ya kushinda nitatimiza malengo yangu ikiwemo kujenga nyumba lakini kuichangia klabu yangu ya Yanga," alisema Kayombo.
Kayombo ameshinda Milioni 188,484,550.
Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amewataka Watanzania waendelee kucheza Perfect 12 huku dau lake likizidi kuongezeka kila mara.
Ukitaka kubeti unafanyaje??
ReplyDelete