February 10, 2019


BEKI kiraka wa timu ya Tanzania Prisons, Salum Kimenya amesema kwa sasa wachezaji wote wanapambana kwa hali na mali kuokoa timu yao isishuke daraja kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Prisons ambayo msimu uliopita ilimaliza ikiwa nafasi ya nne na kocha wao Mohamed Abdalah kuwa kocha bora imeshindwa kuonyesha makali yake msimu huu hali iliyopelekea kocha huyo kupigwa chini.

Kimenya amesema kuwa kikubwa ambacho wachezaji wanakifanya kwa sasa ni kuona wanapata matokeo chanya kwenye michezo yao ya mzunguko wa pili.

"Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa sasa hasa ukizingatia timu yetu haipati matokeo ya kuridhisha, tumeamua kupambana kwa nguvu ili kupata matokeo chanya yatakayotufanya tubaki ligi kuu msimu ujao," amesema Kimenya.

Prisons ambayo ipo nafasi ya 17 kwenye msimamo na pointi 23 wataikaribisha Stand United iliyo nafasi ya 11 ya Shinyanga yenye pointi 29 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic