February 15, 2019


KIKOSI cha KMC leo kitakuwa Uwanja wa Uhuru kumenyana na Kagera Sugar mchezo wa marudiano baada ya ule wa mzunguko wa kwanza kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Ofisa Habari wa KMC, Anuary Binde amesema kocha, Ettiene Ndayiragije amewapa mbinu mpya wachezaji wake zitakazosaidia kuibuka na ushindi.

"Mchezo wetu dhidi ya Alliance tuliacha pointi mbili baada ya sare ya kufungana 1-1 na wapizani wetu wa leo walipoteza mbele ya Ndanda FC, hivyo utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani, imani yangu tutafanya vizuri kutokana na maandalizi ambayo wachezaji wamefanya," amesema Binde.

KMC inashika nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 25 ikiwa imejikusanyia pointi 36 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 17 imecheza michezo 24 na ina pointi 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic