February 15, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umemtaka Msemaji wa Yanga, Dismas Ten kuthibitisha kile alichokiandika katika mtandao wa kijamii 'Instagram' kuwa klabu yao inahusika katika upuliziaji dawa katika vyumba uwanjani.

Kupitia ukurasa wake, Ten aliandika kuwa "wasijifiche kwenye kisingizio cha kumfunga Mwarabu, tabia yao ya kupuliza dawa vyumbani imeshajulikana. Hawatusumbui na safariii hawatoki", kauli ambayo ambayo Manara ameamua kuitilia maanani.

Katika maelezo yake Manara amemtaka Ten kuja na uthibitisho wa kile alichokiandika la sivyo hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yake.



6 COMMENTS:

  1. Yanga wanaanza mchecheto na mapema sio kitu kizuri.

    ReplyDelete
  2. Huyo ten anatafuta umaarufu kwa nguvu awe kama dela boss manara

    ReplyDelete
  3. Naomba Uongozi Wa Simba Ufuatilie Kauli Ya Dismas Ten Kwa Sababu Madawa Hayo Hayaruhusiwi Ktk Soccer Sasa Haiwezekani Mtu Analopoka Na Anaachwa Mm Naomba Adhibitiwe

    ReplyDelete
  4. Ten hana sifa ya u-Afisa Habari / Usemaji. Anakoelekea ni kujipoteza yeye binafsi na pia hata kuiponza timu yake. Maana kwa nafasi yake na aina ya maelezo yake, ni dhahiri ameyatoa kupitia nafasi yake ndani ya Klabu ya Yanga, na si maelezo yenye muono wa maelezo binafsi. Achukuliwe hatua haraka sana!. Huo sio utani wa jadi kwa kauli kama hizo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama Dismas hana sifa basi wewe utakuwa nayo,lete maombi na CV yako tuichubguze kima wee

      Delete
  5. Mapovuuuu mmejulikana Tabia yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic