BAADA ya kucheza na timu zote mbili Simba na Yanga na Yanga, kocha wa Stand United, Amars Niyoganbo amesema leo Yanga itawashangaza wengi.
Simba na Yanga zitamenyana leo Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu mchezo wao wa kwanza.
Niyoganbo amesema wengi hawaipi nafasi Yanga kutokana na mwenendo wake wa mechi za hivi karibuni ila wana kitu cha ziada ambacho kitawashangaza wengi.
"Naiheshimu timu ya Yanga, ni timu kubwa na ukitizama kuelekea kwenye mchezo wao wa watani wengi wanasahau kwamba Yanga inaongoza ligi kwa sasa hivyo sio ya kuibeza hata kidogo itafanya maajabu ambayo wengi hawatarajii.
"Uwezo na kasi yao uwanjani hasa kwa kuweza kubadili matokeo wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri, kwa upande wa Simba kitakachowaponza kama watajiamini kupitiliza baada ya kumfunga mwarabu itakuwa ngumu kupata matokeo hivyo wasiibeze Yanga," amesema Niyogabo.
Tusubiri Dakika 90 Ndo Utakuwa Mwisho Wa Maneno, Maneno Nina Amini Kila Timu Imejipanga Vema Kitakacho Amua Ni Uwezo Binafs Wa Wachezaji Mmoja Mmoja Ndo Utakao Toa Matokeo Ya Leo Na Kutokana Na Hilo Ndo Maana Yanga Ina Bezwa Kwakua Ina Tegemea Wachache Mf. Mchezo Uliopita Beno Kakolanya Ndiye Aliamua Matokeo
ReplyDeleteKila nikitazama naona yanga kukwamuka ni shida, hsa kutokana na kuvunjika moyo kwao kutokana na ahadi za viongozi za mwaka mzima zisizo za kweli kuwa Manji atarejea na huku wakitegemea pesa za bakuli ambazo hazina uhakika wala hazitoshi hata mishahara ya wachezaji wawili na huku wakiwaona akina Bocco nyuso juu kwa furaha ya maisha matamu
ReplyDeleteKatika mechi ya leo ni kweli kabisa Yanga inaweza kuwashangaza wengi lakini vile vile kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kuwasikitisha wengi leo. Kwanza Simba wakifanikiwa kumkamata Ibrahim Ajibu na kumtia mfukoni kwa Yanga itakuwa ni sawa na mtu aliepigwa kabali na kukatwa mawasiliano yake ya pumzi kitu ambacho kwa Simba kumdhibiti Ajibu ni sawa na mama anavyomjulia mwanawe chakula gani anapenda yaani rahisi simba kwao kumdhibiti Ajibu kuliko timu nyingi kwenye ligi kuu bara. Yanga kama wataamua kweli kula sahani moja na Simba yaani kucheza open football sio kupaki kama mechi iliyopita kama alivyoahidi kocha wao basi sifikirii kama yanga atatoka salama taifa.
ReplyDeleteWaache wajiamini sana, wahamasishane kuujaza uwanja Ila wasiwasi no kwamba kuna uwezekano Wa kung'oa viti vyote kwa mchina. Yanga Oyeeeeeeeeee! Pambaneni vijana.
ReplyDelete