GEOFREY Mwashiuya dakika ya 46 aliandika bao la kwanza kwa kikosi chake cha Singida United mbele ya Lipuli hali iliyofanya waamini wataibuka kidedea Uwanja wa Samora, Iringa.
Faulo waliyopata Lipuli dakika ya 65 ilipigwa kiufundi na Haruna Shamte ambaye aliweza kusawazisha mzani na kuweka usawa kwa timu zote mbili.
Kazi iliendelea ampapo Awesu Awesu alitoa pasi ya bao kwa Boniphace Maganga aliyeandika bao dakika ya 84 na kuzifufua upya ndoto za kubeba pointi tatu.
Dakika ya 90 zilikamilika bila Lipuli kuchomoa na mwamuzi aliongeza dakika tatu ikiwa imebaki dakika moja Miraj Athumani alichomoa bao la pili na kuwaacha Singida United wasiamini wanachokiona.
Matokeo hayo yanaifanya Singida United kufikisha pointi 29 ikiwa nafasi ya 15 huku Lipuli wakifisha pointi 38 wakiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.
Offside hio
ReplyDelete