February 6, 2019


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Singida United dhidi ya Yanga kwa sasa ikiwa ni mzunguko wa pili Uwanja wa Namfua, Singida umekamilika kwa suluhu ya bila kufungana.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuona namna mwendelezo wa Ligi unavyoshika kasi kwa sasa.

Kipindi cha kwanza mchezaji wa Singida United Boniphace Maganga alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumzibia njia mlinda mlango Ramadhan Kabwili.

Hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mpinzani mpaka sasa ikiwa ni kipindi cha pili kwa sasa, timu zote zinapambana kutafuta matokeo.

Kipindi cha pili dakika ya 55 Feisal Salum alionyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza rafu, pia nahodha wa Singida United. Kenedy Juma alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 64.

Matheo Anthon alifanyiwa mabadiliko dakika ya 59 nafasi yake ikachukuliwa na Pius Buswita.

Nahodha Ibrahim Ajibu anaingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Feisal Salum, mpira wake wa kwanza ni faulo ambayo ameipasiha mawinguni.

Athanas Adam wa Singida United alifanyiwa mabadiliko dakika ya 64 nafasi yake ikachukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Dakika ya 83 Habib Kiyombo alitoka nafasi yake ikachukuliwa na Frank Mkumbo.

Mvua ilianza kunyesha uwanja wa Namfua dakika ya 86 ya mchezo.

Heritier Makambo mshambuliaji kinara wa mabao Ligi Kuu Bara alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.

5 COMMENTS:

  1. Simba acheni kupiga kelele njoeni kwenye ligi kwanza huwa mnapoteza mechi na timu za mikoani mkiwa taifa kitu cha ajabu Yanga huwa hapotezi mechi taifa na timu za mikoani.

    Ukiona kapoteza Ujue na simba au Azam lakini simba huwa mnapigwa pale pale taifa!

    ReplyDelete
  2. Singida United imelamba kocha wa uhakika.Dragan Popadic amefundisha timu kadhaa Africa ikiwemo Simba na nilimkubali sana na aliondoka Simba kwa mizengwe ileile ya kuingiliwa benchi la ufundi.

    ReplyDelete
  3. Mechi 3 pointi 2.Ingekuwa ni Simba pundits uchwara wametoa kila sababu na makala ndefu zingeandikwa.
    Gari la barafu limeanza kuyeyuka.

    ReplyDelete
  4. Ha ha ha haaaaaaaaaaa, Gari la barafu kweli hili, limekutana na jua, sasa ni hatari tupu. Lenzao li-ice cream cku nyingiiii lilishaanza kupoteza uelekeo na kuyeyuka, nalo lilikutana na nyumba isiyo na friza. Kila mmoja atarudi nafasi yake tu. Muda bado.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic