MENEJA Jurgon Klopp's jana aliiongoza timu yake kurejea kileleni baada ya ushindi wa katika uwanja wa Anfield baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth.
Bao la tatu lililofungwa na Mohamedd Salah linamfanya azidi kuwa wa moto kwa wafungaji kwani anaendelea kuwa namba moja akiwa na mabao 17.
Bado timu ya Liverpool ina nafasi ya kuwa ndani ya timu tatu bora kwenye Premier League kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kama itaendelea na mwendo huu.
Bournemouth wapo kwenye hatari kubwa baada ya kupoteza mchezo wao wa jana mbele ya Liverpool kwani wamebaki na pointi zao 33 wakiwa wamecheza michezo 26.
Liverpool walicheza kwa kushambulia mwanzo mwisho kwenye mchezo wao na walifanikiwa kwa mbinu yao ambayo walikuwa nayo.
Serdio Mane alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 24 na bao la pili lilifungwa na Wijnaldum kabla ya Mohamed Salah kumaliza kazi kwa kufunga bao la tatu.
Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha pointi 65 na kuishusha chini timu ya ManCity ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 62.
0 COMMENTS:
Post a Comment