February 21, 2019


SALIM Aiyee, mshambuliaji wa Mwadui FC, ana mabao 13 kwenye ligi akimpoteza mfungaji bora wa msimu uliopita Emmanuel Okwi wa Simba.

Okwi alipewa tuzo ya mfungaji bora msimu wa mwaka 2017/18 bada ya kufunga mabao 20 mpaka sasa ana mabao saba huku akipotezwa na Aiyee.

Aiyee amesema bado ana kazi ngumu ya kufanya kwa sasa kwenye ligi ili kuisaidia timu yake kupata pointi tatu muhimu.

"Nafurahia kuona timu yetu inapata matokeo ni jambo la kujivunia, bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kwamba tunabaki kwenye ligi msimu ujao.

"Ushirikiano ambao ninaupata kutoka kwa wachezaji pamoja na kufuata maelekezo ya mwalimu kunatufanya tupate matokeo, nitafunga kila ninapopata nafasi," amesema Aiyee.

Mwadui FC wanashika nafasi ya nane baada ya kucheza michezo 28 wakiwa wamekusanya pointi 33.

1 COMMENTS:

  1. Bado sana angalia mwezi huu utapata majibu mchezaji bora na kocha bora ili ujue simba sio ya mchezo mchezo hata afanye nn ataishia njiani huyo.ni sawa na mbumbumbu kukaa kiti cha mbele ukitegemea utaongoza,ngoja zikibaki mechi tano kwa timu zote ndio ulete hii tathmin hapa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic