February 21, 2019


WAZIRI wa Maliasili na Utalii Hamis Kigwangalla amefiwa na mtoto wake anayefahamika kwa jina la Zul, ambapo mazishi yatafanyika kesho saa 10 Wilayani Nzega kwa sasa msiba upo nyumbani kwa Waziri makumbusho nyumba za Mawaziri.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na msiba huo na kuandika “Nimepata maumivu makali baada ya kusikia taarifa ya msiba wa mtoto Zul Hamis Kigwangala. Inna Lillah waina ilaih raajiun. 

Pole sana kwa msiba ndugu yangu Hamis Kigwangalla na mola akupe subra katika mtihani huu mkubwa, mzito sana. Tupo pamoja nawe. Tumshukuru Allah kwa yote”


2 COMMENTS:

  1. Innaa liLlaahi wa Innaa Ilayhi Raajiuun. Allaah awape Subra wafiwa wote, Aamiin.

    ReplyDelete
  2. Pole sana mkubwa. Hii ni njia yetu sote, bali kila mmoja huenda kwa wakati aliopangiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic