MCHEZAJI YANGA: YANGA ILISTAHILI KUFUNGWA 3-0
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Ally Mayay Tembele, amesema kuwa Yanga ilistahili kufungwa mabao 3-0 katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Simba.
Mayay amesema anaamini Simba ilikuwa na uwezo huo kutokana na aina yawachezaji ilionao pia uwezo wa uwanjani.
Mkongwe huyo ameeleza kuwa chachu ya Simba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilitarajiwa kuonekana haswa baada ya kuwafunga waarabu kwa bao 1-0.
Amefunguka kwa nafasi ambazo Simba walizipata kama wangezitumia vizuri wangefanikisha kuibuka na ushindi lakini kukosa umakini kulisababisha washindwe.
Mayay vilevile amengeza kuwa kwa namna pia Yanga walivyokuwa wanachukuliwa pamoja na mapungufu mengi mengi walioyano ingekuwa rahisi kwao kupoteza mechi hiyo.
Hata hivyo Tembele amewapongeza Yanga kwa namna walivyopambana pamoja na mbinu za Mwalimu kuweza kuzuia na kuruhusu bao hilo moja huku alama tatu zikienda Simba.
KWELI KABISA
ReplyDelete