MENEJA mreno mwenye uzoefu ambaye alitimuliwa Manchester United mwezi Desemba amechomoa ofa ya kuifundisha timu ya Benfica ambayo ilikuwa timu yake ya kwanza kufundisha
Mourinho ambaye amekuwa akihusihswa kujiunga na Paris Saint-German (PSG) amefanya kazi Hispania na Italia pia amefundisha England na Ureno kwa sasa anataka changamoto mpya kwenye ligi mpya.
"Najiona mimi mwenyewe nikiwa ni kocha katika Ligue 1, mimi ni mwanaume ambaye nimefanya kazi katika mataifa manne tofauti, naenda kujifunza utamaduni mpya nifanye kazi na mabingwa wengine ili kupata ujuzi zaidi.
"Kwa sasa nimetulia najaribu kuishi na familia yangu na marafiki bado najipa matumaini nitarejea kwenye mpira hivi karibuni. Nadhani kwa sasa ni zaidi ya miezi miwili ama mitatu hivi nakaa bila kazi ila sijali ikiwa zaidi ya hapa kwangu itakuwa ngumu
Ole Gunnar Solskjaer alichukua nafasi ya Mourinho alifanikiwa kutopoteza kwenye mchezo yake 11 ya mwanzo ila alinyooshwa na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora Uwanja wa Old Trafford.
Alipoulizwa kama alibahatika kuutazama mchezo wa Man United dhidi ya PSG amesema hakuwa na muda wa kutazama mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment