February 8, 2019


Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) na Mwekezaji wa timu ya Simba, Mohamed Dewji leo Februari 2019  amewaombamashabiki wa timu ya Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly utakaopigwa Jumanne Februari 12,  2019 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari Mo ametaja kingilio cha shillingi 2000/- na kusisitiza kuwa ndoto yake ni kuona Simba wanakua mabingwa wa kombe hilo na ameahidi kueendelea kuwekeza zaidi katika timu hiyo.

Pamoja na mambo mengine Mo pia amezungumzia matokeo ya mabaya ya simba na kusisitiza nidham kwa wachezaji kuelekea mchezo huo.

2 COMMENTS:

  1. Mo ni jembe hasa yaani ni kiongozi. Kama mwanasimba nilishaishiwa na stamina ya kuisapoti timu yangu ila Muheshimiwa kanijenga upya na kanipa nguvu mpya Asante sana. Hii ndio faida yakuwa na kiongizi na mfumo uliokamilika kwenye taasisi. Hakuna utani kama Simba isungekuwa na mfumo imara wa uongozi hali ingekuwa mbaya sana hivi sasa kutokana na hivi vipigo viwili vya aibu. Asante sana Mo Mungu akulinde na hasada Amin.

    ReplyDelete
  2. Tuweke machungu pembeni, tuelekeeee Taifa kuishangilia timu yetu kama tulivyozoea jamani. Simba Nguvu Moja!.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic