TETEMA YAMFIKISHA RAYVANNY KWENYE RECORD KUBWA KITAIFA, AMPIKU ALIKIBA
MSANII Rayvanny toka kundi la Wasafi Cl;assic Baby (WCB) amefanikiwa kufikia rekodi ya juu baada ya wimbo wake wa ‘Tetema’ video yake kutazamwa mara milioni moja kabla ya masaa 24 katika mtandao wa Youtube.
Wimbo wa Tetema aliomshirikisha boss wake, Diamond Platnumz ,ulifanikiwa kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 17 tu kabla ya masaa 24.
Wanamuziki Diamond Platnumz na Alikiba ni baadhi ya waliofanikiwa nyimbo zao kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 24. Mpaka wakati huu wimbo huo umetazamwa mara milioni 1.2.
Rekodi hiyo inakuwa inampita Ali Kiba 'King Kiba' kupitia wimbo wake wa Kadogo ambao ulifikisha watazamaji milioni 1 baada ya kuchukua takribani siku 5.
0 COMMENTS:
Post a Comment