February 18, 2019


MEZUT Ozil amegoma kuondoka Arsenal licha ya kuelezwa hatakiwi na kocha wake, Unai Emery. Emery amekuwa hafurahishwi na kiwango cha Ozil wakati analipwa mshahara mkubwa wa pauni 350,000 kwa wiki.

Kocha huyo sasa anataka Ozil aondoke ili kupunguza mzigo wa mshahara kwenye klabu na apate kununua wachezaji wengine.

Emery inasemekana amemwambia Ozil kuwa aanze kutafuta timu kwani hamuhitaji kwenye msimu ujao Ozil, 30, inasemekana amegoma kuondoka na anataka kumaliza mkataba wake kwenye klabu hiyo Paris St. Germain ilitaka kumchukua kwa mkopo wakati wa kipindi cha dirisha dogo la usajili la mwezi Januari lakini Ozil aligoma kuondoka.

Ozil ameanza mechi moja tu kati ya 10 za hivi karibuni na hakusafiri na timu wakati ilipokwenda Belarus kwenye mechi ya Ligi ya Europa na kufungwa 1-0 na BATE Borisov, Alhamisi iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic