February 28, 2019


Klabu ya Singida United imefanikiwa kumpelekea mchezaji John Tibar George namba 7 Mgongoni kwenye club ya Mfk Fc iliyopo Jamhuri ya Czech.

Tibar ameondoka usiku wa jana saa 5 akipitia Ufaransa ambako atakaa kwa muda usiopungua wiki moja kwenye club Toulouse Fc kwaajili ya fitness na techniques.

Vibali vyote vimeshatumwa kwenye klabu yake mpya ikwepo ITC. Hivyo anakwenda huko kuanza maisha ya soka moja kwa moja.

Tunashukuru sana wote waliohusika kufanikisha hili, zaidi TFF kwa ushirikiano wao wote katika kipindi chote cha kuhakikisha vibali vya mchezaji huyu vinapatikana kwa wakati.

Huu ni mwendelezo wa Singida United kuendelea kuwafungulia njia wachezaji wakitanzania kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania. Tutaendelea kufanya hivi kwa maslahi ya, klabu, timu ya Taifa na wachezaji wenyewe.

1 COMMENTS:

  1. Wasije wakawa wanakwenda kupotea kama akina Farid Musa. Banda tunamsikia South. Msuva Moroco .Himid Misry lakini hao we gone hatusikii chochote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic