MWIGULU AWAITA VIRUKA NJIA WANAINYIMA UZALENDO SIMBA, AWATAKA WAENDA TAIFA KESHO
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amewaita mashabiki wale wasiionesha uzalendo kwa klabu za Tanzania kuwa viruka njia.
Nchemba ameeleza hayo jana wakati klabu ya Simba ikiwa inajiandaa kuwakabili Al Ahly ya Misri katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.
Simba itakuwa inacheza mchezo huo wa kundi D ikiwa na kumbukumbu za kupigwa mabao 5-0 huko Misri, mechi iliyokuwa ya raundi ya kwanza.
Nchemba amesema mashabiki wa timu zingine kwa ujumla wanapaswa kuiunga mkono Simba ili kuipa morali na motisha ya kufanya vizuri.
Kiongozi huyo anaamini uwezekano wa kuifunga Al Ahly utakuwepo kwasababu wanatumia Uwanja wa nyumbani.
"Mashabiki wasiounga mkono timu za nyumbani zikicheza mashindano ya kimataifa hao ni viruka njia, naamini Simba wanaweza kupata matokeo kwani hata Al Ahly walishinda kwao na Simba inaenda kucheza kwenye Uwanja wa nyumbani" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment