Yanga imeamua kuishia Morogoro kikitokea Tanga na kuweka kambi maalum kujiandaa dhidi ya Simba ambapo timu hizi zitakutana Jumamosi ya wiki hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Tayari Kocha Zahera ameshaanza kuwapa tizi la maana vijana wake kuhakikisha kuwa wanapambana na kuchukua alama tatu dhidi ya Simba ambao nao wanapigania kutetea taji la ligi.
Kambi hiyo inawafanya Yanga washindwe kuwashuhudia Simba Uwanja wa Taifa ambapo watacheza dhidi ya Al Ahly leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba atakuwa anacheza kipute hicho cha Ligi ya Mabingwa Afrika na kisha baada ya hapo maandalizi dhidi ya Yanga yataanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment