SAKATA LA KAKOLANYA NA YANGA LACHUKUA TASWIRA NYINGINE
LICHA ya kuomba kuvunjiwa mkataba wake na Klabu ya Yanga, kipa Beno Kakolanya atalazimisha kusubiri baada ya mwanasheria wa klabu hiyo kupata safari ya nje.
Kakolanya amewasilisha maombi ya kutaka kuvunjwa kwa mkataba wake na Yanga baada ya kutokea hali ya kuwekwa pembeni kuichezea timu hiyo.
Upande wa Kakolanya waliwasilisha maombi hayo ambapo juzi Jumatano viongozi wa Yanga walikuwa watoe majibu.
Mwanasheria wa Kakolanya, Leonard Richard ameliambia Championi Ijumaa kwamba, kwa sasa zoezi hilo la uvunjwaji wa mkataba huo wa Kakolanya na Yanga umeshindikana baada ya mwanasheria wa upande wa Yanga kusafiri.
“Walikuwa wana dhamira hiyo ya kuvunja mkataba lakini wamesema mwanasheria wao amesafiri atarudi Jumamosi na uwezekano wa kuandika barua kabla ya Jumamosi itakuwa ngumu.
“Kwani Jumapili wana mechi wa ligi mkoani Tanga na wao viongozi wanaenda huko akiwemo mwenyekiti ambapo watarudi Jumatatu.
“Wamesema tusubiri mpaka Jumanne ijayo ndiyo tutafahamu imefikia wapi, nimeona busara kufanya hivyo, baada ya hapo Jumanne kama hawatajibu tutaenda sehemu nyingine,” alisema mwanasheria huyo.
Wakati huohuo, Kakolanya ameanza mazoezi maalumu ya gym kwa ajili ya kulinda kiwango chake. Kipa huyo ameliambia gazeti hili kuwa, anafanya mazoezi mara mbili kwa siku katika gym na uwanjani ili kuweka sa
0 COMMENTS:
Post a Comment