Ikumbukwe mara ya mwisho katika mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Simba ilifanya maandalizi yake kwenye Uwanja wa Boko Veterani na kuahirisha safari ya kwenda visiwani Zanzibar.
Simba haitoweza kusafiri kwenda popote kwani itakuwa na siku chache baada ya mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly kumalizika Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi wanakabiliwa na mechi hiyo kubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo watapaswa kupambana kusaka alama tatu ili kujiwekea nafasi nzuri ya kufika hatua ya robo fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment