SINGIDA UNITED WAIPA PRESHA YANGA, YAMSHITAKI MMOJA BODI YA LIGI
Klabu ya Singida United imeandika Barua ya Malalamiko kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Kuhusu Uhalali wa kutumika kwa Mchezaji Wa Yanga Sc Gustava Simon.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida, Festos Sanga, amesema Simon alicheza mchezo huo akiwa hana leseni inayomtambulisha kuwa ni mcheza wa Yanga.
Sanga amefunguka kwa kusema Simon ana leseni ya ligi daraja la kwanza pekee hivyo Yanga hawakuwa na uhalali wa kumtumia.
Malalamiko ya Singida United ni kwamba Gustava Amecheza Mchezo wa Leo ikiwa Leseni yake inaonesha ni Mchezaji wa Klabu ya Dar City inayoshiriki ligi daraja la kwanza. "Tumeandika barua na Tumeambatanisha Vielelezo vyote Juu Ya kiungo Gustava" - Festo Sanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment