February 8, 2019


Kaimu Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Tandale kwa Mtogole, Waziri Jitu, ameibuka na kukanusha taarifa ya kuwa alisema anamtishia maisha Kocha wa timu yake, Mwinyi Zahera.

Jitu amesema kuwa hakuna ukweli wowote licha ya kumsikia Zahera mwenyewe akimtaja kuwa amepanga kumuangamiza kisa Yanga kutokuwa na mwenendo mzuri.

Kiongozi huyo ameeleza kwamba hakusema kama Zahera alivyokuja na kuongea mbele ya vyombo vya habari bali yeye ndiye anamtetea Kocha huyo juu ya watu kadhaa wanaopingana na kazi yake katika timu.

Jitu amefunguka kwa kusema amekuwa akipingana na baadhi ya wadau kadhaa wa Yanga ikiwemo wanachama wanaopanga mipango ya kumharibia Zahera jambo ambalo limekuwa halimfurahishi hata kidogo.

Amemtaja Mwenyekiti wa Usajili Yanga, Hussein Nyika, kuwa anahusika katika uchakachuaji wa timu na njama za kuifanya Yanga iharibu ili Zahera aondolewe akisema pia Nyika amekuwa akimtangaza Jitu ili aonekane mbaya.

Ikumbukwe Zahera juzi alisema kuna mtu anaitwa Jitu amemtishia maisha, kauli ambayo Jitu mwenyewe ameikanusha kwa kusema hakuwa na maana hiyo.

"Napingana na kauli hiyo, si kweli kama nilisema Zahera nitamtishia maisha, nimesema namtetea Zahera sababu kuna genge linaloongozwa na Hussein Nyika ili kumharibia kazi Kocha, naungana na Zahera kwasababu anapiga kazi ya maana na napenda aendelee zaidi kuifundisha Yanga" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic