BAO la Meddie Kagere wa Simba, alilopachika wavuni dakika ya 64 dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika lilitosha kuwamaliza waarabu na kubakiza pointi tatu Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ulikuwa ni wa marudio kwa Simba baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kuchapwa mabao 5-0, wao leo wameamua kumuonjesha joto ya jiwe.
Iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 64 baada ya mashambulizi ya muda mrefu kushindwa kuzaa matunda.
Zana Coulibary ikiwa ni mchezo wake wa kwanza alianzisha mashambulizi pembeni kwa kumpa pasi John Bocco ambaye alituliza kwenye kifua na mpira kumfikia Kagere aliyemalizia kwa shuti lililozama ndani ya wavu.
Kwa ushindi huo Simba wanakusanya pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi sita wakiwa kundi D huku Al Ahly wakibaki na pointi zao saba wakiwa nafasi ya kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment