March 19, 2019



KOCHA wa timu ya AS Vita Florent Ibenge amesema kuwa ameshangazwa namna alivyofungwa na kikosi cha Simba Uwanja wa Taifa kwani alijiandaa kushinda kwenye mchezo huo uliowapoteza mazima kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ibenge ambaye ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Congo, kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Congo alishinda kwa mabao 5-0 hali iliyomfanya aamini angetumia nguvu hiyo kutinga hatua ya robo fainali.

Ibenge amesema kuwa kwenye mchezo huo alianza vizuri na wachezaji wake walijitimu ila baada ya kufunga bao la kwanza walijisahau wakadhani wapo nyumbani hali iliyowapa nafasi Simba kusawazisha.

"Tulianza kwa mipango mikali ya kutafuta bao la mapema na hilo tulifanikiwa, wachezaji wangu walijisahau wakadhani tumeshinda hali iliyowapa nafasi wapinzani wetu kusawazisha.

"Kwenye chumba cha kubadilishia nguo niliwapa mbinu mpya ila zote ziligoma na nikashanga mpira unaisha tumefungwa mabao 2-1, lakini yote ni matokeo hivyo nawapongeza Simba maana tuliwafunga nyumbani kwetu na wao wametufunga," alisema Ibenge.

3 COMMENTS:

  1. Ebana we! Kwa mara ya kwanza tangu nianze kuwafuatilia As vita kuwaona wakionekana wanyonge. As vita ni wababe nje na ndani ya uwanja lakini Mazingira ya uwanja wa Taifa yaliwafanya wakongo kukosa kujiamini kwa kila walichokuwa wakitaka kufanya mpaka wengine mikojo ikiwatoka hadharani. Nimeamini kuwa Simba ni timu kubwa na watanzania tukiamua kufanya kweli uwezo tunao asikwambie mtu. Vita huyu aliemtandika TP MAZEMBE tatu mtungi 3-0 juzi tu leo alikuwa akiomba mpira uishe mbele ya Simba uthibitisho gani tena watanzania tunautaka wa kuamini kuwa uwezo tunao tukiamua na kilichobaki ni kujiamini tu.

    ReplyDelete
  2. Kufuatia ushindi wa Simba mengi yanazungumzwa ndani na nje ya nchi. Wengi Duniani wakisema As vita wamekutana na Surprise Tanzania lakini ninachokiamini mimi muda si mrefu Tanzania ndio itakayokuwa the perfect surprise of all around the globe. Yaani muda si mrefu Tanzania inaelekea kuwa mshangao kamili duniani kote. Kama kasi hii ya utendaji ya serikali ya awamu ya tano itaendelea na kuongezeka basi nchi yetu na watu wake itawashangaza wengi.Moja ya hutuba zake za hivi karibuni raisi wa Marekani alisema baba yake alikuwa mjenzi na alimfundisha kwa kumwambia yakwamba kiongozi hakuna atakacho kikamilisha kwa kukaa ofisini.Na kama msimamizi wa ujenzi basi lazima kiongozi awepo kwenye site kusimamia kabla hata jengo halijasimama ili kujiridhisha ubora wa vifaa vitakavyolinyanyua jengo hilo kwani kuja kulikagua jengo lilokwisha nyanyuliwa na kubaini mapungufu gharama yake ya kulivunja na kulijenga tena upya ni kubwa mno na ni upotevu wa muda. Kwa kifupi raisi wa Marekani alisema..You can't get rich by staying behind the Desk.Nimetoa mfano huu ili kumpongeza kiongozi wetu wa nchi Muheshimiwa John Magufuli kiroho safi kabisa kwa jitihada zake binafsi za kuwaendeleza watanzania na Tanzania. Hata hizi hamasa tulizonazo leo kama Taifa kuhusiana na uthubutu wa simba kwenye mashindano haya makubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu barani Africa chanzo chake ni kauli ya kujiamini ya Muheshimiwa raisi kuwataka Simba kubeba kombe la klabu bingwa Africa. Kwa kiasi fulani sisi watanzania tunashindwa kuelewa kwa kiasi gani Mungu ametupendelea kuwa na kiongozi wa uwezo wa uongozi aliaonao Magufuli. Kwa watanzania na Taasisi za kitanzania zitakazofuata maelekezo ya Muheshimiwa raisi Magufuli kwa ufasaha hakika lazima zitapiga hatua kwani vitu vingi anavyoongea ni vya kweli kabisa. Tusishangae kabisa watanzania tukajatukaona kuna nchi fulani inapiga hatua kwa kufuata mikakati ya Magufuli sisi tukibakia kupiga siasa za hovyo zisizo na tija. Kwa watanzania wanaompinga au kubeza juhudi zake wajue tu kuwa wao sio wa kwanza kukaidi na kupotosha juhudi za Mwenyezi Mungu za kuwaletea wanadamu kiongozi anaekuwa na manufaa nao ila wajue wapo kwenye lilopotoka. Hata Jesus aliuwawaa lakini kwa unafiki wa mwanadamu hata kama jambazi akiguswa kidogo na machungu eti Oh Jesus? Hakuna mkamilifu ila wanaongozwa wakipata fursa ya kuwa na kiongozi anaejali hali zao za maisha kuliko hata hali yake yeye mwenyewe binafisi basi kiongozi huyo ni wa kutunzwa na kuenziwa na kusikilizwa kwa makini sana. Nilipata nafasi ya kumsikiliza Muheshimiwa spika wa Bunge akiulezea ushindi wa Simba na faida zake ya kuitangaza nchi hasa katika nyanja ya utalii.Nampongeza sana Muheshimiwa Ndugai kwa uweledi wake juu ya faida ya michezo katika kuitangaza nchi, unaweza kusema michezo huitangaza nchi bila ya gharama lakini faida zake ni kubwa hasa kwa nchi kama Tanzania iliosheheni vivutio vya kitalii. Kwa kusisitiza Tanzania peke yetu tunao uwezo wa kuandaa African cup of nations na tujikite zaidi katika kuvitangaza vivutio vyetu vya kitalii. Wenzetu huandaa mashindano makubwa kama haya ili kujipa challenge binafsi ya kuinua hadhi ya miji yao hasa katika sekta ya miundo mbinu.kwa Tanzania kituo kama cha mwanza,Arusha,Dodoma,Dareslaam na Zanzibar iwe ni miji ya kimikakati ya kuindaa kwa ajili ya kuandaa African cup of nations itakuja kutulipa kunako long term hasa kunako shirika letu la ndege na utalii ni kijipanga tu.

    ReplyDelete
  3. Haya Yanga hawakuamini kilichotokea walienda kwa wingi wa makundi wakitegemea Simba kufungwa...Nilifuatilia Moira kwa radio..Mara baada ya goli LA kwanza kufungwa nilidhani ni Simba wamefunga kumbe ni kelele nyingi za kushangilia za mashabiki wa AS Vita ambao ni wa hapahapa Tanzania!Hawakuamini Chama alipowaharibia matumaini yao dakika ya mwisho.Hongereni Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic