March 18, 2019



CLATOUS Chama wa Simba ameitikisa Afrika kwa kutupia mabao ya usiku na muhimu kwa timu yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Chama aliyesajiliwa na Simba msimu huu, ameonekana kuwa mchezaji muhimu kwa kufunga mabao hayo yanayoifanya mpaka sasa Simba kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Simba ilipata tiketi ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ambapo cheche za Chama zilianza kuonekana kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatin kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kwenye mchezo huo, Simba ilishinda mabao 4-1 ambapo Chama alifunga bao la nne dakika ya 90 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.

Pia kwenywe mchezo wa marudiano uliochezwa nchini Eswatin, Chama alifunga mabao mawili dakika ya 27, 31 na alitoa pasi ya bao kwa Meddie Kagere dakika ya 62 kwenye ushindi wa mabao 4-0.

Katika mchezo wa mtoano dhidi ya Nkana FC, Chama alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mkude dakika ya 29, bao la tatu ambalo lilikuwa la ushindi alifunga dakika ya 88 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga kwenye ushindi wa mabao 3-1 kwenye  Uwanja wa Taifa.

Hatua ya makundi mchezo wao wa kwanza dhidi ya JS Saoura, Uwanja wa Taifa, Chama alitoa pasi ya bao lililofungwa na Okwi dakika ya 45 kwenye ushindi wa mabao 3-0.

Alimaliza kuonyesha thamani ya uwepo wa mashabiki juzi dhidi ya AS Vita, Chama aliipeleka tena Simba hatua ya robo fainali baada ya kufunga bao dakika ya 90.

Hivyo mpaka sasa Chama amefunga mabao matatu dakika za lala salama huku mawili yakiivusha Simba kwenye hatua muhimu, ametoa jumla ya pasi tatu za mabao ndani ya Simba kimataifa akiwa na jumla ya mabao matano kwa sasa.

1 COMMENTS:

  1. Hakika Chama anaujua mpira wakati mwengine unaweza kusema kana kwamba benchi la ufundi la Simba hawajajua bado jinsi ya kumtumia vizuri kwani mara nyingi humuweka chama mbali na goli la mpinzani lakini ni mchezaji asiekata tamaa ya ushindi na anaonekana kuwa na njaa ya kuipatia ushindi Simba kama vile katokea academi ya Simba. Ukiangalia karibu mara zote kwenye mechi anazongara chama kunakuwepo na kiungo kazi mwengine uwanjani kama vile khasani Dilunga na hii inampa nafasi chama kusogea mbele zaidi karibu na goli. Juzi kwenye mechi ya As vita uwepo wa Haruna Niyonzima aliekuwa kwenye ubora wake kulimpa nafasi chama kusogea galini zaidi na kufanya yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic