March 19, 2019


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swed Nkwabi, amesema kuwa kikosi chao kinapaswa kufanya usajili ili kujiweka fiti zaidi katika hatua ya ligi ya mabingwa Afrika ambayo wametinga hivi sasa.

Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali Jumamosi ya wiki jana kwa kufanikiwa kuitandika AS Vita ya Congo kwa bao 2-1, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi Nkwabi ameeleza kikosi kinaweza kusajili wachezaji wengine ili kuendana na ukubwa wa hatua waliyopo maana si ya mchezo.

"Tunajua changamoto za mashindano haya na hatua tuliyofikia kuna uwezekano wa kusajili wachezaji wengine walio bora zaidi ili kuweka nguvu kikosini.

"Tunazidi kuomba sapoti na hamasa iendelee kwa wapenzi na mashabiki zetu kwani bila wao hatuwezi kufika popote."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic