DEPAY AING’ARISHA UHOLANZI, WATUPIA BAO 4-0
MEMPHIS Depay akiwa ndani ya jezi ya Uholanzi ameonyesha kiwango bora na kufanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Belarus.
Timu hizo zilikutana katika mchezo wa makundi kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Euro 2010, matokeo ambayo yamemfanya Kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman kuwa na mwanzo mzuri katika mchakato huo ulioanza juzi usiku.
Depay ambaye ni staa wa zamani wa Manchester United, alifunga mabao hayo katika kila kipindi huku mabao mengine yakifungwa na Georginio Wijnaldum na Virgil van Dijk. Ushindi huo wa Kundi C umeifanya Uholanzi kuongoza kundi hilo kabla ya mchezo mwingine wa Ujerumani.
Kwa mabao hayo sasa Depay ambaye alikuwa Mchezaji Bora wa Mechi amefi kisha mabao 10 katika mechi 14 za kimataifa alizoichezea timu yake ya taifa. Mchezo mwingine wa Kundi C, Ireland ya Kaskazini nayo ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Estonia, michezo yote ikichezwa usiku wa juzi.
Katika Kundi E, Croatia ilishinda 2-1 dhidi ya Azerbaijan, Slovakia ikaifunga Hungary mabao 2-0. Kundi G, Austria ikiwa nyumbani ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Poland, Macedonia ya Kaskazini ikashinda mabao 3-1 dhidi ya Latvia, Israel na Slovenia zikatoka sare ya bao 1-1. Kundi I, Kazakhstan 3-0 Scotland, Cyprus 5-0 San Marino, Ubelgiji 3-1 Urusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment