BEKI wa timu ya Yanga, Abadlah Shaibu 'Ninja' amesema licha ya kikosi chake kupoteza mbele ya Lipuli mchezo wa ligi bado wana nafasi ya kubeba ubingwa ulio mikononi mwa Simba kwa sasa.
Ninja amesema kuwa kupoteza mchezo kwenye ligi haina maana ya kupoteza kasi ya kuendelea kupambana bali ni matokeo ambayo yanaikuta timu yoyote inayotafuta ushindi.
"Bado naiona timu yangu ikibeba ubingwa wa ligi msimu huu hivyo kupoteza kwetu mbele ya Lipuli hakujatuyumbisha bali kumetupa hasira ya kupambana kuyatafuta mafanikio.
"Bado tuna michezo mikononi na bado tunaongoza ligi sioni kitakachotufanya tupoteze kwa sasa hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti, wachezaji bado tuna nguvu na matumaini ya kufanya makubwa," amesema Ninja.
Yanga wamecheza michezo 28 wamepoteza michezo mitatu pekee na wametoa sare michezo minne kwenye ligi huku wakiwa ni vinara wa ligi baada ya kukusanya pointi 67 kibindoni.

Unayosema ni yakweli tupu na hakuna wakupinga kwasababu timu yenu ipo kwenye kiwango bora na baadae kuyafanya waliyoshindwa wana simba kuyafanya pamoja na kuleta ubingwa wa Africa. Mungu azidi kuibariki yanga
ReplyDelete