March 16, 2019



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unaingia kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Lipuli kwa tahadhari kubwa kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye ligi.

Yanga watakaribishwa na Lipuli Uwanja wa Samora ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wanatambua kwamba Lipuli ni timu imara hasa ikiwa nyumbani hivyo wanaingia kwa tahadhari kubwa.

"Wapinzani wetu wapo vizuri hasa Uwanja wa nyumbani, rekodi zao zinawabeba hivyo hilo tumelifanyia kazi tutaingia kwa tahadhari kubwa kutafuta pointi tatu.

"Lengo letu ni kuona tunapata matokeo chanya ili tujiweke kwenye nafasi nzuri, tunahitaji pointi tatu muhimu na hilo linawezekana kutokana na morali ya wachezaji." amesema Saleh.

Lipuli wameshinda mbele ya Mbao FC uwanja wa nyumbani mchezo wao wa hivi karibuni pia walilazimisha sare na Singida United pamoja na Azam FC ambao walikuwa kwenye ubora wao.


3 COMMENTS:

  1. Ikiwa hawatogungwa yanga mpaka mchezo wao wa mwisho na simba pia kumaliza bila ya kufungwa basi simba itaizidi yanga kwa pointi nane RAHAA

    ReplyDelete
  2. picha ya simba ya nini asubiri mziki wa azam mechi mbili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic