March 15, 2019


Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya AS Vita, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amemuona Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kukaa karibu na Wakongo ili kuwapa mbinu.

Kupitia kipindi cha Sports HQ cha Radio EFM, Manara ameongea kimafumbo bila kutaja jina la Zahera akidai kuwa amesalia Dar es Salaam kuwapokea Vita na hajasafiri kwenda Iringa na timu yake.

Manara ameeleza kuwa Kocha huyo amekuwa akizunguka na Vita jijini Dar es Salaam bila kujua kama anapaswa kuwa na majukumu ya kuisaidia timu yake ambayo ina mechi na Lipuli Jumamosi hii huko Iringa.

Ofisa huyo amemuona Zahera kuwa makini na anachokifanya kwa sababu hii ni mechi ya kimataifa na kitaifa.

"Hii ni mechi ya kitaifa na ya kimataifa, tunaiwakilisha nchi, kuna kocha yeye kazi yake imekuwa ni kuzunguka na Vita tu na aliaga anaenda kwao Congo hata Iringa hajaenda.

"Hii ni mechi ambayo nchi inajua, Rais anajua, sasa ole wake aendelee kutuharibia mipango."

11 COMMENTS:

  1. Manara acha uoga play football Bana. Wakimwaga mboga wewe kamwage ugali, Simba sio timu ya taifa japo twatakiwa kuwa wazalendo kwa kusupport. Ingekuwa timu ya Taifa ndo ungekuja na hayo maneno. Easy bro USHINDI NI JUHUDI

    ReplyDelete
  2. Kamwe huwezi kumuona Gaurdiaola wa Mancity akiisapoti wazi wazi Barcelona pale Uengereza inapokwenda kucheza na timu za Uengereza kwani anajua kitu hicho kinaweza kumugharimu hata ukaazi wake achilia mbali kazi yake.Lakini Zahera ameshaona kuwa watanzania wenyewe hawajielewi.Usishangae kusikia yakuwa viongozi wa Yanga ndio waliomuomba Zahera kubakia Daresalam kuisadia As Vita kupata ushindi zidi ya Simba yaani ni hovyo kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli, wakati Barca wanaenda kucheza na Liver Gardiola mbona aliongea na akina Mess? Unajua kuwa Casillas wa RM alikuwa na urafiki na wachezaji wa Barca na kila siku walikuwa wanachart hata kabla ya game baina yao? Acheni mawazo mgando, mpira sio vita.

      Delete
  3. Acheni ujinga, Toka mwanzo Zahera alishasema hatoenda Iringa kwakuwa anajiandaa kwenda Congo kwenye timu ya taifa na akasema hataki usumbufu kila kitu aulizwe Mwandila. Huwezi kumzui mtu kuongea na watu wa kwao kisa ni timu pinzani. Tumeona wachezaji wa timu pinzani wakiongea na kucheka hata kabla ya game na bado haiondoi ushindani. Hayo ni mawazo mgando ya mwaka 47. Wakati wanafungwa 5. Zahera alikuwepo? Mpira haufundishwi kwa siku moja na wala mbinu za kimpira sio fedha kwamba utampa mtu mwingine akusaidie kuwasilisha.

    ReplyDelete
  4. Wamejikita kweli kumpa sapoti kocha wao. Zahera kaikwepa timu yake
    yanga na akaamua abaki Dar,Salam awe pamoja na timu ya nyumbani kwao. Ni haki yake na haiwezekani kumlaumu kwasababu damu ni nzito kuliko maji

    ReplyDelete
  5. tz hakunaga hyo kitu "uzalendo" tunaona wagen kila wakija wanapata support ya timu pinzan, au simba yake watadai washawahi kuja taifa kuishangilia yanga hadi imuume zahera kukaa na ndugu zake bhakongo?

    ReplyDelete
  6. zahera nmusengeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerema au mkongo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic