March 15, 2019


Uongozi wa klabu ya Simba umewataka wanachama na wapenzi wake kuhakikisha wanaanza kukaa uwanjani upande wa kusini badala ya kaskazini kama ilivyozoeleka.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amewataka wanasimba kuhakikisha wanajaza nafasi hizo ili kuwapa wakati mgumu watani zao wa jadi kuja kukaa upande huo.

Manara amesema lengo lao ni kuifanya mechi isiwe ya nyumbani na badala yake iwe ya nyumbani pekee.

Kauli hiyo imekuja kutokana na mashabiki wamekuwa na utamaduni wa kuja uwanjani kushangilia wapinzani kisha kuizomea Simba jambo ambalo amesema Manara halitakiwi kufanyika kwa kesho.

Simba itacheza mechi hiyo majira ya saa 1 za usiku na ili kuingia hatua ya robo fainali inapaswa kupaswa matokeo na si vingine.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic