March 18, 2019


MWENYEKITI wa kamati ya uhamasishaji kwa ajili ya kuichangia Yanga, Antony Mavunde amewataka wananchi kuendelea kuichangia timu ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Mavunde amebainisha mipango iliyopo kwa sasa ambayo ni kufanikiwa kuchangia zaidi ya shilingi 1.5 bilioni kutoka wa wanachama na mashabiki wa Yanga mikoa yote nchini.

Yanga kwa sasa inajiendesha kutokana na nguvu ya michango ya wanachma kutokana na kupita kipindi cha mpito.

Ili kuichangia Yanga kupitia mitandao ni kupitia namba hii *150*01# kisha chagua namba 4 lipa bili, hatua inayofuata chagua namba 3 weka namba ya kampuni ambayo ni 101120, kumbukumbu namba weka namba 1 kisha weka kiasi kisipungie mia tano, weka namba ya siri kuhakiki kisha utapokea Ujumbe wa kuthibitisha.

4 COMMENTS:

  1. Tatizo ni kukosekana uhamasishaji na kutokuwa na watu wa kuaminika ambao wana Yanga wanaweza kuwaamini kuwa wakituma hela zao basi zitakuwa kwenye mikono salama.Ushauri wangu kwa Mavunde na kamati yote kwa ujumla;kabla hamjaanzisha hili vuguvugu la "Make Yanga Great Again"ni vizuri mkateua watu maalum wenye heshima yao katika jamii ambao watakabidhiwa jukumu la kuhusika na akaunti maalum ya michango,kuna watu wengi wenye mapenzi mema na Yanga kama vile Mzee Mengi,Mzee J.M.Kikwete,Ridhiwani Kikwete,Freeman Mbowe,Mwigulu Nchemba,George Mkuchika,Rostam Aziz,Charles Boniface na wengineo ambao watakabadhiwa jukumu la kudhibiti michango na pia akaunti iwe ni kwa ajili ya usajili wa wachezaji na mishahara tu.Nina hakika Yanga haikosi wanachama laki tano tu(500,000)ambao wakihamasishwa vema na kuchangia shilingi elfu mbili kwa kila mwezi uhakika wa kupata Shilingi Billion Moja kwa mwezi unawezekana kikubwa ni kwamba kuwe na uhakika wa hela za wana Yanga kuwa kwenye mikono salama.HAKUNA LISILOWEZEKANA,NI KUAMUA TU......Kama Watanganyika waliweza kumchangia Mwalimu Nyerere nauli na posho akweza kwenda UNO itashindikana vipi wana Yanga kuichangia timu yao!!!!!!MAKE YANGA GREAT AGAIN!!!!!

    ReplyDelete
  2. Washabiki na wanachama wa yanga wameamua kuichangia Simba tunashukuru wanavyojaa kwenye mechi zetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanajaa kushangilia AS Vita na JS Soura Al Ahly wakitegemea mnyama atafungwa kumbe wanaishia kuumia!

      Delete
  3. Lakini hivi karibuni tulipata habari za kutia moyo kuwa Zahera alifanya mazungumzo na Manji na kuwa faraja haipo mbali na baadhi ya mashabiki tukafurahi sana na tukaamuwa kusita kujitolea je huo ulikuwa ni uvumi tuu lakini juu ya hayo tupo tayari kujitolea kwa hali na kwa mali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic