MWENYEKITI wa kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, Paul Makonda amewataka mashabiki wote Tanzania bila kujali itikadi kuanzia wale wa Simba, Yanga, Lipuli, Azam, Mbeya City na timu zote wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu ya Taifa siku ya jumapili Uwanja wa Taifa.
Stars ambayo kwa sasa ipo kambini itashuka Uwanjani tarehehe 24 mwezi Machi kumenyana na timu ya Uganda ambayo tayari imefuzu Afcon itakayofanyika nchini Misri mwaka huu mwezi Juni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Makonda amesema kuwa nguvu kubwa ya mafanikio ni sapoti kwa mashabiki hasa kwenye timu yetu ya Taifa bila kujali itikadi za ushabiki.
“Mafanikio ya Taifa Stars ndiyo mafanikio ya Tanzania katika michezo, Jumapili tutacheza kwenye Uwanja wetu wa Taifa dhidi ya Uganda hivyo kila mmoja anapaswa kumwambia shabiki mwenzake aje na kuhudhuria mchezo wetu, kama juzi tuliutikisa Uwanja kwa nini tushindwe kuujaza kwa timu ya Stars?.
"Mashindano haya ya Afcon hii mechi ni muhimu sana kwani kupitia hii mechi ni daraja la maana sana kwa Taifa letu, tunaamini ni haki yetu kutinga hatua ya Afcon.
"Viongozi wa dini, wasanii, wanasiasa, kila mmoja ambaye anakipaji chake kokote kule kutumia fursa kufanya jambo hili liwe la kwetu sote, uzalendo ni muhimu katika hili kuanzia kwa viongozi, wasanii,tuna matumaini makubwa kwa kocha na wachezaji wetu, Afcon 2019 tutaingia," amesema Makonda.
0 COMMENTS:
Post a Comment