March 15, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema beki kiraka wa Simba, Erasto Nyoni atakuwepo kwenye mchezo wa kesho lakini atamkosa Juuko Murshid.

Nyoni ameanza kufanya mazoezi baada ya kupona jeraha la kwenye mguu alilopata mwezi Januari kwenye michuano ya Mapinduzi.

Aussems amesema Nyoni alifanya mazoezi tangu wiki iliyopita ingawa hakukusafiri kwenda Algeria ila bado ana nafasi ya kuwa ndani ya kikosi chake kesho.

"Nyoni tulianza naye mazoezi hivyo imani yetu tutakuwa naye kwenye kikosi cha kesho kitakachowavaa AS Vita.

"Kuhusu Juuko bado anahitaji mapumziko mpaka Jumatatu kwa hiyo kwa uhakika Juuko hatakuwepo katika timu," amesema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic