KINDOKI AUTAJA UCHAWI YANGA
Kipa aliyechukua namba ya Ramadhani Kabwili hivi sasa, Mkongomani, Klaus Kindoki, amesema kuwa kiwango chake kiliporomoka akiamini kuwa watu walikuwa wanamfanyia mambo ya kishirikina, imeelezwa.
Taarifa imesema kipa huyo amefunguka na kueleza wakati anaanza kazi Yanga alikuwa anapitia wakati mgumu zaidi mpaka kufikia hali ya kukata tamaa kufanya kazi yake.
Kindoki amesema inawezekana kuna watu walikuwa wanamroga kwakuwa kila alichokuwa anakifanya uwanjani kilikuwa hakina maana.
Ameeleza kuna wakati alikuwa akijiona uwanjani kama yupoyupo tu na kupelekea lawama nyingi kwake kutoka kwa wanachama na wapenzi wa Yanga.
Aidha, Kindoki amewataja wachezaji wenzake kuwa walikuwa wakimfuata na kumhoji juu ya kiwango chake kilivyokuwa mwanzo huku wakimtia moyo.
Tayari hivi sasa Kindoki amejihakikishia namba ndani ya kikosi cha Yanga baada ya Kabwili aliyeumia hivi karibuni.
Dhana zisizpkuwa na mana na kupitwa na wakati
ReplyDelete