March 19, 2019


Kikosi cha Simba kinaingia dimbani majira ya jioni leo kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting FC.

Simba inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa imetoka kufuzu na kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga AS Vita ya Congo kwa mabao 2-1.

Kuelekea mechi ya leo Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems, amesema atatumia kikosi mchanganyiko kutokana na wale wengine kuitwa timu za taifa.

Kocha huyo amesema kikosi cha leo kitakuwa mchanganyiko kwa sababu wengine tayari wameshajiunga na timu za taifa kwa ajili kuwania kufuzu fainali za AFCON mwaka huu.

Licha ya nyota wake hao kutokuwepo, Aussems anaamini wanaweza kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting kutokana na upana wa kikosi chake.

7 COMMENTS:

  1. Kikowapi hicho kikosi hujakitaja

    ReplyDelete
  2. Hii bodi kweli itabeba lawama bure itakuwaje wachezaji wameshakwenda kwenye majukumu ya kitaifa halfu ninyi mnapambana na ligi?, halafu bahati mbaya wakifungwa lawama za nani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashangaa kwamba je kanuni imekikuwa au Simba ndio wameridhia?

      Delete
    2. Mbona simba wakatiwenzao wanacheza ligi wao walikuwa wakifanya maandalizi mengine?????

      Delete
    3. Mbona simba wakatiwenzao wanacheza ligi wao walikuwa wakifanya maandalizi mengine?????

      Delete
    4. hivi unajua unachoongea wachezaji wengi wako kwenye majukumu ya timu za taifa na timu ikiwa na wachezaji kuanzia watatu kwenye timu ya taifa mechi zao zinasimamaishwa

      Delete
  3. Naamini watakao pata nafasi leo watafanya vyema sana, Ruvu Shooting wateja wetu wa kudumu hata Bwire analitambua hilo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic