March 18, 2019

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa haina namna licha ya kutinga hatua ya robo fainali juzi kwa kikosi cha Simba kwa kuitungua AS Vita mabao 2-1 kesho watakaa mbele ya kikosi chake.

Bwire amesema kuwa ana imani na maandalizi ya kikosi chake hivyo kesho ni suala la muda tu kukipoteza kikosi cha Simba  Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

"Wanasema kituo kinachofuata ni Ruvu Shooting, kituoni ni lazima ushushe abiria hiki kituo kinachofuata ni kikubwa zaidi, kina heshima zake,  lazima abiria ashuke, abaki kituoni hapo wao waendelee na safari zao, abiria anayebaki ni pointi.

"Simba kituo hiki lazima mfe pointi mtaziacha sisi ni zaidi ya Mbao, kumfunga AS Vita hakuwafanyi muifunge Ruvu Shooting, mpira hauko hivyo.

"Kwa udhibiti huu ni lazima ndani ya Sen'genge za nondo nene hivi mtafurukuta kwa mfano mtakufa kama Simba aliyeuliwa na shujaa Samson porini kati ya Gadha na Timma nyie mtafia pale kwenye nyasi za Mkapa, March 19,2019 kuanzia saa 1:00 jioni shughuli ya kuwang'oa sharubu itakapoanza.Noto itawezesha papasa Squared iwang'oe mpaka magego," amesema Bwire.

1 COMMENTS:

  1. Bwiri lugha kama hiyo huzidi kumtia ukali na kumpa ghadhabu mnyama simba na bora muingie kimyakimya na huenda akakuonea huruma

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic