March 19, 2019


Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems ameingiwa na wasiwasi juu ya wachezaji wake kutokana na mazoezi ya mara mbili kwa siku wanayofanya katika kikosi cha Taifa Stars.

Tayari timu hiyo imeshaingia kambini na imeshaanza maandalizi ya mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda utakaopigwa Machi 24 jijini Dar es Salaam.

Aussems amesema mazoezi ya mara mbili kwa siku yanaweza sababisha wachezaji wake wapatwe na uchovu zaidi kwani wanakabiliwa na mashindano ya kimataifa.

Ameeleza mazoezi hayo yatawapa uchovu zaidi wachezaji hao huku akiomba ni vizuri zaidi wakirejea wakiwa salama ili kuendelea na harakati za kupambana na ubingwa.

Simba ina wachezaji wanne katika kikosi cha Taifa Stars ambao ni Jonas Mkude, Aishi Manula, John Bocco pamoja na Erasto Nyoni na wengine wa kimataifa wakiwa washasafiri kuelekea kwao ikiwemo Emmanuel Okwi.

4 COMMENTS:

  1. Nakumbuka mwaka jana na kocha ni huyuhuyu Amonica, wachezaji waliokuwa katika kambi yake alikuwa akiwaruhusu kujiunga na vilabu vyao pale inapokuwa wana mechi za ligi, jee safari hii mambo yamebadilika?

    ReplyDelete
  2. Tafadhali mtoa maoni hapo juu japo kocha humpendi lakini jina lake sio a Monica bali ni Amunike. Kocha wa Simba lazima aingiwe na hofu juu ya wachezaji wake kwenye kambi ya taifa stars kwani tayari ilishaigharimu Simba na Tanzania moja ya mchezaji muhimu sana kwa sasa Shomari kapombe. Ninavyofahamu mimi timu ya taifa yeyote ni sehemu ya mkusanyiko wa wachezaji waliokwisha iva tayari kikubwa ni kuwafanya kuwa kitu kimoja hayo mambo ya mazoezi ya pre-season kwa kweli ni kama kituko.

    ReplyDelete
  3. Baada ya kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa wachezaji wa Simba wamepanda thamani hakuna ubishi.
    Unapozungumzia wachezaji wa Simba hivi sasa unazungumzia mitambo ya hela wazungu wanaelewa hilo. Sasa wanapoona mtu anajaribu kuiendesha mitambo hiyo kibongobongo lazima wataguna. Kule Simba wana wataalam wao wa mazoezi kutoka nje waliospecilize katika masuala ya mazoezi ya mwili tu. Sasa sidhani kama taifa stars wana watu kama hao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa kaka kwakweli inakuwaje ipigishe watu mazoezi ya mara mbili na huku umeita watu waliokuwa wakitumika kwenye ligi mpaka hatu ya mwisho? maana hapo unawapa mbinu tu sasa mazoezi yanakuwa ya kawaida tu, hapa mtake msitake lazima tena watu waumie maana wanaingia kwenye mechi washajichokea angalia maandalizi ya uganda hata kwenye Mtandao huko misri ni kama wanakula bata sasa sisi mazoezi kama vile pre-season na huku mechi ni baada ya siku nne tu kwa nn wasichoke na kuumia?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic