March 19, 2019


Kitendo cha Yanga kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa huko Iringa Jumamosi iliyopita, kimezidi kuwapa nguvu zaidi Simba ambao wana viporo vingi mkononi.

Kwa mujibu wa Kocha, Patrick Aussems, amesema kupoteza kwa watani zao wa jadi kunazidi kutoa morali kwa vijana wake kupigania ubingwa wa ligi.

Aussems ameeleza kuwa Simba hivi sasa itakuwa na nguvu zaidi kwa kuchagizwa na namna walivyotinga hatua ya robo fainali kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

"Kupoiteza kwa Yanga kutazidi kutoa morali kubwa kwa wachezaji wetu kufanya vema kwenye ligi.

"Tunatumia faida hiyo kuelekea mechi yetu na Ruvu Shooting ambayo tutatumia wachezaji mchanganyiko kwa kuwa wale wa kikosi cha kwanza wengi wako timu za taifa".


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic