March 17, 2019


KOCHA mkuu wa klabu As Vita Club ya DR Congo, Florent Ibenge anaamini Yanga itatwaa ubingwa msimu huu katika Ligi Kuu Bara sababu tu ina kocha bora na mwenye uwezo.

Yanga kwa sasa inafundishwa na kocha Mkongo, Mwinyi Zahera ambaye ni rafiki mkubwa wa kocha Ibenge na wanafanya kazi pamoja katika timu ya DR Congo na wanaishi mtaa mmoja Ufaransa.

“Yanga safari hii watafanikiwa kutwaa ubingwa wao wa ligi kuu sababu wana kocha bora ambaye yuko makini na kazi yake na ninamfahamu vyema na hilo halinipi shaka hata kidogo.

“Sababu Zahera ni mtu wa kazi na analielewa vyema soka, hivyo sina wasiwasi naye katika hilo naona hata timu yake nafasi iliyopo kwa sasa katika ligi, wanaongoza kutokana na ubora wa mwalimu waliyenaye.

“Na sioni sababu ambayo itamfanya ashindwe kutwaa ubingwa mpaka hapo alipofikia sasa, yule ni rafiki yangu namfahamu vyema hata katika utendaji wake wa kazi,” alisema Ibenge ambaye ni rafiki mkubwa wa Nicholas Anelka wa Ufaransa.

5 COMMENTS:

  1. Pumbafuuu..mnapeana siri za ujinga..tunasikia hata juzi AS Vita walipofika walipewa siri na mjinga Zahera..Haya endeleeni kupatiana siri za kindombolo ya solo!

    ReplyDelete
  2. na angefungwa simba mngesema zahera ndie amewapa siri sababu hamtumii akili
    na hiki kisingizio kilishatayarishwa mapema kabla ya mchezo kama simba itashindwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga wanatumia akili ambazo haziwafikishi popote...miaka yote...Haya wakipata viingilio huwanjani hawatumii akili katika matumizi ya pesa...matokeo kutembeza kopo

      Delete
  3. Wanapeana Moyo lakini zahera anajua kuwa sio rahisi hata kama ni kocha mzuri je anawachezaji wazuri?

    ReplyDelete
  4. Hawa wakongo Wapo sawa kichwani kweli.inakuwaje awadanganye yanga kuwa watachukua ubingwa!!!!,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic